Swalah iliyompita mtu anailipa haraka iwezekanavyo

Swali: Mtu amepitwa na swalah kutokana na udhuru. Je, inafaa kuichelewesha baada ya kuondoka udhuru?

Jibu: Haijuzu kuchelewesha swalah nje ya wakati unapoondoka udhuru. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule mwenye kupitikiwa na usingizi au akaisahau swalah, basi aiswali pale atapoikumbuka. Haina kafara nyingine isipokuwa hiyo.”[1]

Amefanya wakati wa kuilipa ni pale inapokumbukwa. Ukiichelewesha wewe ni mwenye kupata dhambi.

[1] al-Bukhaariy (597) na Muslim (684).

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/224)
  • Imechapishwa: 04/08/2026