Swali: Msichana akianza kupata hedhi sehemu ya mwezi wa Ramadhaan ni lazima alipe sehemu nyingine iliyompita? Ikiwa sio lazima, je, ni lazima kulipa zile siku ambazo alikula kwa sababu ya hedhi?

Jibu: Akianza kupata hedhi amebaleghe. Ikiwa kama alikuwa hajapata alama zingine za kubaleghe zaidi ya hedhi hii, bi maana alikuwa hajafikisha miaka kumi na tano, hajaota nywele za chini na wala hajaota na kumwaga manii kwa matamanio, bali amejiwa na hedhi tu pindi yuko na miaka 10, 11 au mfano wa hayo, ahesabu kuwa ni hedhi. Hivyo ni juu yake kufunga kuanzia pale alipobaleghe. Akianza kupata hedhi mwisho wa Sha´baan, ni lazima kwake kufunga Ramadhaan nzima. Akipata hedhi katikati ya Ramadhaan, anapaswa kufunga baada ya kutwaharika ikiwa atatwaharika na bado Ramadhaan ipo. Atafunga zile siku ambazo zitakuwa zimebaki na atalipa zile siku ambazo alipata hedhi [na akawa amekula] kwa kuwa amebaleghe.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://ramadhan.af.org.sa/ar/node/6481
  • Imechapishwa: 23/09/2020