2839- Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Kumbukeni kifo wakati wa kuswali kwenu. Kwani hakika mtu anapokumbuka kifo wakati wa kuswali kwake basi anapata funzo la kuswali vizuri. Swali swalah ya mtu ambaye hajui kama atakuja kuswali swalah nyingine. Tahadhari na kila jambo ambalo utajipa udhuru kwalo.”

Ameipokea ad-Daylamiy katika ”Musnad-ul-Firdaws” kupitia kwa Abush-Shaykh Ibn Hayyaan, Ibn Abiy ´Aaswim ametuhadithia: Baba yangu ametuhadithia: Shabiyb bin Bishr ametuhadithia, kutoka kwa Anas, kutoka kwa Mtume wa Allaah.

Cheni ya wapokezi ni nzuri.

Baadhi ya maimamu wana mazowea ya kuwaamrisha waswaliji pindi wanaposimama katika safu:

صلوا صلاة مودع

”Swalini swalah ya kuaga.”

Naona hakuna neno neno kufanya hivo baadhi ya nyakati, ama kuchukulia ndio mazowea na daima ni jambo la kizushi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Ahaadiyth as-Swahiyhah (6/2/821)
  • Imechapishwa: 20/07/2020