Swali Sunnah baada ya swalah ya faradhi

Swali: Nimeanza kuswali Rak´ah mbili kabla ya swala ya Fajr. Tamahaki kukakimiwa swalah ilihali nimeshaswali Rak´ah moja. Je, inafaa kwangu kuikamilisha au nijiunge na swalah ya faradhi?

Jibu: Hapana, unatakiwa kuikata. Ukianza Rak´ah moja na kukakimiwa swalah basi ikate. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kukikimiwa swalah basi hakuna swalah nyingine isipokuwa ile ya faradhi.”

Ataiswali baada ya hapo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24772/ماذا-يفعل-من-اقيم-للفريضة-وهو-يصلي-نافلة
  • Imechapishwa: 12/12/2024