Namna inavyolipwa swalah ya ´iyd kwa aliyekosa

Swali: Ikiwa mtu atakosa swalah ya ´iyd kwa mujibu wa maoni yanayosema kuwa ni faradhi ya kutosheleza atairudia mtu peke yake?

Jibu: Ni bora kuirudia. Lakini ikiwa tutasema ni wajibu wa kila mtu binafsi, basi ni lazima kuilipa. Lakini kwa mujibu wa maoni yanayosema kuwa ni faradhi ya kutosheleza ya kwamba ni Sunnah, basi inapendeza kuilipa kwa kuswali Rak´ah mbili.

Swali: Ikiwa ikiwa mtu katika swalah ya ´iyd atapitwa na Rak´ah moja?

Jibu: Ataongeza Rak´ah moja kama ilivyo kwenye swala ya ijumaa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24770/حكم-قضاء-صلاة-العيد-لمن-فاتته
  • Imechapishwa: 12/12/2024