21. Maswahabah walikuwa wakitafuta mwezi mwandamo

Swali 21: Waislamu wote wanapata dhambi ikiwa hakuna yeyote katika wao aliyefanya bidii ya kuutafuta mwezi mwandamo wa Ramadhaan ni mamoja ikiwa kuanzia au kumalizika kwake?

Jibu: Kutafuta mwezi mwandamo – mwezi wa Ramadhaan au mwezi wa Shawwaal – ni jambo lilizoeleka katika zama za Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum). Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhum) amesema:

“Watu walitoka nje kuona mwezi mwandamo. Nikamweleza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba nimeuona. Kwa hivyo akafunga na akawaamrisha watu wafunge.”[1]

Hapana shaka kwamba uongofu wa Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) ndio kamilifu zaidi.

[1] Abu Daawuud (2342). Ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”al-Irwaa´” (908).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: 48 mas-alatu fiy Swiyaam, uk. 29-30
  • Imechapishwa: 19/04/2021