20. Wamejua kuwa mwezi umeandama katikati ya mchana

Swali 20: Ni lazima kwa watu kujizuia siku iliobaki ikiwa wamejua kuanza kwa mwezi baada ya kupita sehemu ya wakati wa mchana?

Jibu: Watu wakijua kuwa mwezi umenza katikati ya mchana basi ni lazima kwao kujizuia. Kwa sababu imekwishathibiti kuwa siku hiyo ni ya mwezi wa Ramadhaan hivyo basi ni lazima kujizuia. Lakini ni lazima kulipa siku hiyo? Wanachuoni wametofautiana katika jambo hili. Jopo la wanachuoni wengi wanaona kuwa ni lazima kuilipa. Kwani hawakunuia kuanzia sehemu ya mwanzoni mwa mchana. Imekwishawapitikia sehemu ya mchana pasi na manuizi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika kila kitendo kinategemea na nia na kila mmoja atalipwa kwa kile alichonuia.”[1]

Baadhi ya wanachuoni wengine wameona kuwa si lazima kulipa. Kwa sababu walikuwa ni wenye kula kwa ujinga na mtu asiyejua ni mwenye kupewa udhuru kutokana na ujinga wake. Lakini kulipa ndio salama na lenye kutakasa zaidi dhimma ya mtu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Achana na lile linalokutia shaka na kuliendelea lile lisilokutia shaka.”

Ni siku moja na ni nyepesi na haina ugumu wowote. Jengine ni kwamba kulipa kunaipumzisha nafsi na kuipa moyo utulivu.

[1] al-Bukhaariy (01) na Muslim (4962).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: 48 mas-alatu fiy Swiyaam, uk. 22
  • Imechapishwa: 19/04/2021