Swalah za faradhi zinalipwa wakati wowote

Swali: Vipi mtu atalipa swalah ya Maghrib au swalah ya Fajr inapompita mtu wakati wa kuchomoza kwa jua au kuzama kwake?

Jibu: Swalah iliyompita mtu inalipwa katika wakati wowote na hakuna kikwazo juu yake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule atakayepitiwa na usingizi ambapo akapitwa na swalah au akaisahau, basi aiswali atakapoikumbuka. Haina kafara isipokuwa hiyo.”

Fuqahaa´ watano wamesema ni kulipa zile swalah za faradhi. Ni lazima kulipa zile swalah za faradhi hata kama ni katika zile nyakati zilizokatazwa kuswali ndani yake.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalish-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.mufti.af.org.sa/ar/content/كيفية-قضاء-صلاة-المغرب-أو-الفجر-إذا-فاتت-عند-شروق-الشمس-أو-عند-غروبها
  • Imechapishwa: 11/06/2022