Swali: Kuna maoni tofauti kwenye madhehebu katika baadhi ya mambo. Je, madhehebu yepi ni mepesi zaidi katika hayo? Nichague madhehebu gani?

Jibu: Madhehebu yote manne ni haki. Wenye nayo ni wanazuoni na watu wabora. Wanaweza kutofautiana katika ufahamu wa Aayah au Hadiyth. Ni tofauti inayofaa kwa sababu inatokana na Ijtihaad na haitokani na tamaa na matamanio. Lakini sisi tumeamrishwa kufata Qur-aan na Sunnah. Imamu yeyote tunayemfuata ni lazima kutazama maoni yake. Ikiwa maoni yake yanaafikiana na Qur-aan na Sunnah ni haki. Na yule ambaye maoni yake yanatofautiana na Qur-aan na Sunnah hatuyatendei kazi pamoja na kumpa udhuru kwa kwenda kwake kinyume. Hatulazimiki kufuata madhehebu maalum. Kinachotulazimu ni kufuata Qur-aan na Sunnah na kuwaigiliza wale wanazuoni ambao tunawaamini katika dini na elimu yao muda wa kuwa haijanibainikia kuwa wameenda kinyume na haki.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalish-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.mufti.af.org.sa/ar/content/فتاوى-على-الهواء-13-11-1435هـ-0
  • Imechapishwa: 19/06/2022