Swali: Je, inafaa kwa mwanamke kuswali na vifuniko vya mikono?

Jibu: Asivae vifuniko vya mikono akiwa yuko katika Ihraam. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwanamke katika Ihraam asivae Niqaab wala vifuniko vya mikono.”[1]

Hata hivyo inafaa kwake kuvaa vifuniko vya mikono akiwa nje ya Ihraam, ni mamoja ndani au nje ya Ihraam. Bali bora kwake kuvaa vifuniko vya mikono kwa sababu kunamsitiri zaidi na kunamlinda zaidi na fitina.

Hapa kuna jambo ambalo nataka kulizindua: Ikiwa mwanamke anaswali pambizoni na wanaume wasiokuwa Mahram zake, basi ajifunike uso wake ili wasiweze kumuona. Akienda katika Sujuud, basi atafunua uso wake. Dalili ya hilo ni maneno yake Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anh):

“Tulikuwa tukiswali pamoja na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwenye joto kali. Asipoweza mmoja wetu kumakinisha paji lake la uso ardhini, basi hutandaza nguo yake na akasujudia juu yake.”[2]

Zingatia pale aliposema “Asipoweza mmoja wetu kumakinisha paji lake la uso ardhini”. Hii inafahamisha kuwa kitendo hicho hakifanyi isipokuwa tu wakati wa dharurah.

[1] al-Bukhaariy na Muslim. Tazama ”Swahiyh Abiy Daawuud” (1600).

[2] al-Bukhaariy (1207) na Muslim (191).

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/298)
  • Imechapishwa: 09/08/2026