Ameswali kwa kupinda kidogo kutokana na Qiblah

Swali: Ikimbainikia mtu kwamba alipinda kidogo kutokana na Qiblah. Je, airudie swalah yake?

Jibu: Kupinda kidogo haidhuru. Hili linahusu pasipokuwa msikiti Mtakatifu. Katika msikiti Mtakatifu mswaliji anatakiwa kuielekea Ka´bah kabisa. Kwa ajili hiyo wanazuoni wamesema kuwa ambaye anaweza kuiona Ka´bah basi analazimika kuielekea kabisa. Kwa hivyo mswaliji akiswali katika msikiti Mtakatifu pasi na kuielekea Ka´bah ipasavyo kabisa, basi anapaswa kuirudia swalah yake kwa sababu haikusihi. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

قَدْ نَرَى تَقَلُّبَ وَجْهِكَ فِي السَّمَاء فَلَنُوَلِّيَنَّكَ قِبْلَةً تَرْضَاهَا فَوَلِّ وَجْهَكَ شَطْرَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ وَحَيْثُ مَا كُنتُمْ فَوَلُّواْ وُجُوِهَكُمْ شَطْرَهُ

“Hakika Tumeona unavyogeuzageuza uso wako mbinguni, basi Tutakuelekeza Qiblah kinachokuridhisha. Hivyo basi uelekeze uso wako upande wa Msikiti mtakatifu; na popote mtakapokuwepo basi zielekezeni nyuso zenu upande wake.”[1]

Lakini mtu akiwa mbali kabisa na Ka´bah na hawezi kuiona, hata kama atakuwa Makkah, basi ni wajibu kuelekea upande wa Ka´bah. Katika hali hii haidhuru kitu ule upindaji mdogo. Kwa ajili hiyo amesema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kuhusu kuwaambia wakazi wa Madiynah:

“Baina ya mashariki na magharibi ni Qiblah.”[2]

Wakazi wa Madiynah wanaelekea kusini. Kwa hivyo kila kwa upande wao upande wote kati ya mashariki na magharibi ni Qiblah. Kwa wale wanaoswali kwa kuelekea magharibi kwamba upande wote baina ya kusini na kaskazini ni Qiblah.

[1] 2:144

[2] at-Tirmidhiy (342) na Ibn Maajah (1011). al-Haakim ameisahihisha katika ”al-Mustadrak” (1/255) na adh-Dhahabiy akaafikiana naye.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/413-414)
  • Imechapishwa: 09/08/2026