122 – Ikiwa mtu atatembelea kaburi la kafiri, basi asimtolee salamu na wala asimwombee du´aa, bali ampe bishara ya Moto. Hivo ndivo ameamrisha Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Hadiyth ya Sa´d bin Abiy Waqqaas ambaye ameeleza:
“Mbedui mmoja alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: ”Hakika baba yangu alikuwa akiwaunga ndugu, alikuwa hivi na vile. Yuko wapi?” Akasema: ”Yuko Motoni.” Ni kana kwamba mbedui huyo aliathirika na jambo hilo, akasema: ”Ee Mtume wa Allaah, basi baba yako yuko wapi?” Akasema: ”Popote utakapopita karibu na kaburi la kafiri, basi mpe bishara ya Moto.” Akasema: ”Kisha yule mbedui akaingia katika Uislamu baada ya hapo ambapo akasema: ”Hakika Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amenikalifisha jambo gumu. Sijawahi kupita karibu na kaburi la kafiri isipokuwa nilimpa bishara ya Moto.”
Ameipokea at-Twabaraaniy katika ”al-Mu´jam al-Kabiyr” (1/191/1), Ibn-us-Sunniy katika ”´Amal-ul-Yawmiy wal-Laylah” (na. 588) na adh-Dhwiyaa´-ul-Maqdisiy katika ”al-Ahaadiyth al-Mukhtaarah” (3331) kwa cheni ya wapokezi Swahiyh. al-Haythamiy (1/117-118) amesema:
“Ameipokea al-Bazzaar na at-Twabaraaniy katika ”al-Kabiyr” na wanaume wake ni watu wa Swahiyh.”
Ameipokea Ibn Maajah (1/476–477) kwa njia hii hii, lakini ameifanya kuwa ni katika cheni za wapokezi za ´Abdullaah bin ´Umar. al-Buuswayriy amesema katika ”az-Zawaa-id” (98/2):
“Cheni yake ya wapokezi ni Swahiyh na wanaume wake ni waaminifu.”
Lakini ni dhaifu. Kilichohifadhiwa ni kwamba ni cheni za wapokezi wa Sa´d, kama nilivyobainisha katika ”as-Silsilah Ahaadiyth-is-Swahiyhah” (18).
Hadiyth hii kuna nyingine inayoitia nguvu kutoka kwa Abu Hurayrah kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa tamko lisemalo:
”Mnapopita karibu na makaburi yetu na makaburi yenu ya watu wa kipindi kabla ya kuja Uislamu, basi wapeni khabari ya kwamba wao ni miongoni mwa watu wa Motoni.”
Ameipokea Ibn-us-Sunniy katika ”al-Yawm wal-Laylah” (587) kwa cheni ya wapokezi ambayo ndani yake yumo Yahyaa bin Yamaan, ambaye kumbukumbu yake ni mbaya, kutoka kwa Muhammad bin ´Umar, ambaye sikumjua kutoka kwa Abu Salamah kutoka kwake. Lakini dhahiri ni kuwa yeye ni (Ibn ´Amr) na kwamba kosa lilitokea wakati wa kuchapisha. Hadiyth zake ni nzuri.
Yote tuliyoyataja katika masuala haya ndio madhehebu ya Hanaabilah, kama ilivyo katika ”Kashshaaf-ul-Qinaa´” (2/134) na mengineyo katika vitabu vyao.
- Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 251-252
- Imechapishwa: 09/08/2026

Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 251-252
Imechapishwa: 09/08/2026
https://firqatunnajia.com/131-makatazo-ya-kumuombea-duaa-kafiri-wakati-wa-kutembelea-kaburi-lake/