121 – Lakini asilielekee kaburi wakati wa kuliombea du´aa, bali aelekee Ka´bah. Yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kuswali kuelekea makaburi, kama itakavyokuja. Du´aa ni kiini na roho ya swalah, kama inavyojulikana. Hivyo inakuwa na hukumu ya swalah. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Du´aa ndio ´ibaadah.”
Kisha akasoma:
وَقَالَ رَبُّكُمُ ادْعُونِي أَسْتَجِبْ لَكُمْ
“Mola wenu Amesema: “Niombeni, Nitakuitikieni.”[1]
Ameipokea Ibn-ul-Mubaarak katika ”az-Zuhd” (10/151), al-Bukhaariy katika ”al-Adab al-Mufrad” (714), Abu Daawuud (1/55 – kwa maelezo ya al-‘Awn), at-Tirmidhiy (4/178, 223), Ibn Maajah (2/428-429), Ibn Hibbaan (2396), al-Haakim (1/491), Ibn Mandah katika ”at-Tawhiyd” (q 69/1), na Ahmad (4/167, 271, 276, 277). al-Haakim amesema: “Cheni yake ya wapokezi ni Swahiyh” na adh-Dhahabiy akaafikiana naye. Mambo ni kama alivosema. at-Tirmidhiy amesema: “Hadiyth ni nzuri na Swahiyh.” Ameipokea vilevile Abu Ya´laa kwa njia ya al-Baraa’ bin ‘Aazib kama ilivyo katika ”al-Jaamiy´ as-Swaghiyr.”
Katika mlango huo kuna Hadiyth kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anh) kwa tamko lisemalo:
“Du´aa ndio kiini cha ´ibaadah.”
Ameipokea at-Tirmidhiy (2234) ambaye amesema: “Hadiyth ni ngeni kwa muundo huu na hatuitambui isipokuwa kutoka kwa Ibn Luhay´ah.”
Ni dhaifu kutokana na udhaifu wa kumbukumbu yake. Hivyo haijengewi hoja isipokuwa tu pale ambapo itakuwa imesimuliwa na mmoja katika wale wanaoitwa ”´Abdullaah” kutoka kwake, hapo ndipo itatumiwa kama hoja ambapo hii si miongoni mwa Hadiyth hizo. Hata hivyo maana yake ni sahihi kutokana na ushahidi wa Hadiyth ya an-Nu´maan.
at-Twaybiy amesema katika maelezo yake:
“Ametumia dhamiri ya Fasl na khabari yenye Laam ”… ndio ´ibaadah” ili kuonyesha ukomekaji na kwamba ´ibaadah siyo kitu kingine tofauti na du´aa.”
Wengine wamesema: ”Maana ni kwamba du´aa ni miongoni mwa ´ibaadah zilizo kubwa kabisa. Kwa hiyo ni kama kutoa maelezo yanayosema:
”Hajj ni ´ibaadah.”
Kwa maana ya kwamba nguzo yake kubwa zaidi. Hiyo ni kwa sababu ya kuonyesha kuwa mwenye kufanya du´aa anaugeuza uso wake kwa Allaah na akivipa mgongo vingine vyote visivyokuwa Yeye, kwani ameamrishwa kufanya hivyo. Kutekeleza amri ni ´ibaadah. Ameita du´aa kuwa ni ´ibaadah ili mwenye kuomba du´aa aonyeshe unyenyekevu wake, udhalili wake na haja yake, kwani ´ibaadah ni unyenyekevu, udhalili na umasikini.”
Ameyataja hayo al-Munaawiy katika ”al-Faydhw”.
Ikiwa du´aa ni miongoni mwa ´ibaadah kubwa kabisa, basi vipi mtu aelekeze du´aa yake kinyume na mwelekeo alioamrishwa kuelekea katika swalah? Kwa ajili hiyo miongoni mwa mambo yaliyothibitishwa kwa wanazuoni watafiti wa kina:
“Haitakiwi kwa mwenye kuomba du´aa kuelekea upande isipokuwa ule ambao anaelekea wakati wa kuswali.”
Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema katika ”Iqtidhwaa’-us-Swiraatw al-Mustaqiym Mukhaalafati Aswhaab-il-Jahiym”, uk. 175:
“Hili ni msingi wa kudumu kwamba haipendezi kwa mwenye kuomba du´aa kuelekea isipokuwa kule ambako hupendeza kuswali. Huoni kwamba mtu wakati alipokatazwa kuswali kwa kuelekea upande wa mashariki au mwingineo, hivyo basi akakatazwa pia kuelekea upande huo wakati wa kuomba du´aa. Baadhi ya watu huzingatia wakati wa kuomba du´aa kuelekea upande wa mtu mwema aliyekufa, ni mamoja iwe ni mashariki au pengine, jambo ambalo ni upotofu wa wazi na shari bayana, kama vile baadhi ya watu wanajiepusha na kugeuza mgongo upande wa mtu mwema, ilihali hugeuzia mgongo Nyumba ya Allaah na kaburi la Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mambo yote haya ni miongoni mwa Bid´ah zinazofanana na dini ya manaswara.”
Ametaja kabla ya hapo kutoka kwa Imaam Ahmad na wanafunzi wa Maalik kuwa kilichoweka katika Shari´ah ni kuelekea Qiblah wakati wa kuomba du´aa hata ukiwa kwenye kaburi la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) baada ya salamu, jambo ambalo ndio maoni ya ash-Shaafi´iy pia. Imaam an-Nawawiy amesema katika ”al-Majmuu´” (5/311):
”Imaam Abul-Hasan Muhammad bin Marzuuq az-Za´faraaniy – ambaye alikuwa miongoni mwa wanazuoni wahakiki[2] – katika kitabu chake cha ”al-Janaa-iz” amesema:
“Asielekei kaburi kwa mkono wake na wala asilibusu.”
Akasema:
“Namna hiyo ndio Sunnah imepitishwa.”
Akasema:
“Kupapasa makaburi na kuyabusu, kama wafanyavyo wajinga hivi leo, ni miongoni mwa mambo yaliyozuliwa kwa mujibu wa Bid´ah ambayo yanapaswa kuepukwa na kumkataza yule anayefanya hivo.”
Akasema:
“Mwenye kukusudia kutoa salamu kwa maiti, basi atamsalimia upande wa uso wake. Akitaka kuomba du´aa, basi atahama mahali pake na kuelekea Qiblah.”
Hayo ndio madhehebu ya Abu Haniyfah pia. Shaykh-ul-Islaam katika ”al-Qaa´idah al-Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah”, uk. 125:
“Madhehebu ya maimamu wanne – Maalik, Abu Haniyfah, ash-Shaafi´iy na Ahmad na wengine wa maimamu wa Uislamu – ni kwamba mtu anapomtolea salamu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na akataka kujiombea du´aa mwenyewe, basi atageuka kuelekea Qiblah. Wamekhitalifiana juu ya wakati wa kumtolea salamu. Maalik, ash-Shaafi´iy na Ahmad wamesema kwamba mtu ataelekea kaburi na kumtolea salamu moja kwa moja. Abu Haniyfah amesema kwamba asielekei kaburi wakati wa kumtolea salamu kama ambavyo hapasi kuelekea wakati wa kumwombea du´aa kwa maafikiano yao. Katika madhehebu yake kuna mitazamo miwili:
1 – Kuna wanaosema kwamba alipe mgongo kaburi.
2 – Wengine wakasema kwamba alifanye kuwa upande wake wa kushoto.
Haya ndio makinzano yao wakati wa salamu. Kuhusu wakati wa du´aa hakuna makinzano yoyote kuwa mtu anapaswa kuelekea Qiblah, si kaburi.”
Sababu ya tofauti iliyotajwa ni kwamba kaburi tukufu pindi lilipokuwa nje ya msikiti na Maswahabah walikuwa wakimsalimia, haikuwezekana kwa yeyote kumuelekea kwa uso wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kugeuzia Qiblah mgongo wake[3], kama ilivyowezekana baada ya kaburi hilo kuingia ndani ya msikiti baada ya zama za Maswahabah. Basi mwenye kutoa salamu miongoni mwao akielekea Qiblah, basi kaburi linakuwa upande wake wa kushoto, na akisema alielekee kaburi, basi Qiblah kilikuwa upande wao wa kulia na upande wa magharibi ukiwa nyuma yao. Shaykh-ul-Islaam amesema katika ”al-Jawaab al-Baahir”, uk. 14 baada ya kutaja maana hii:
“Wakati huo ikiwa walikuwa wakimwelekea yeye na kugeuzia magharibi migongo yao, basi maoni ya jopo kubwa ndio yenye nguvu zaidi, na ikiwa wataelekea Qiblah wakati huo na kulifanya kaburi kuwa upande wa kushoto wao, basi maoni ya Abu Haniyfah ndiyo yenye nguvu zaidi.”
Shaykh (Rahimahu Allaah) ameliacha suala hili kuwa lenye kuning´inizwa. Hakuhukumu kuwa walikuwa wakielekea upande huu au ule, kana kwamba ni kwa sababu ya kutokuwepo kwa mapokezi yaliyothibiti kutoka kwao kuhusu jambo hilo. Lakini lau tungechukulia kuwa walikuwa wakimuelekea, basi umeshajua kuwa katika hali hiyo walikuwa wakigeuzia magharibi migongo yao wala si Qiblah, kwa sababu hilo halikuwezekana kwao katika zama zao. Tumetangulia kusema kwamba wanazuoni wengi wanasema kwamba inafaa kumkabili uso wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakati wa kumtolea salamu, kitu ambacho kinapelekea kugeuzia mgongo Qiblah, jambo ambalo tunajua kwa hakika hakikutokea katika zama za Maswahabah, kama ilivyotangulia. Hili ni jambo la ziada juu ya kulielekea kaburi, hata hivyo linahitaji dalili ya kuthibitisha. Je, ipo? Mimi sijaijua wala sijamwona mwanachuoni yeyote akiizungumzia, ni mamoja iwe inahusiana na kaburi la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) au juu ya makaburi mengine kwa jumla. Ni kweli baadhi ya watu wametegemea katika hilo Hadiyth ya Ibn ´Abbaas:
Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipita katika makaburi ya Madiynah ambapo akawakabili kwa uso wake na kusema:
السلام عليكم يا أهل القبور، يغفر الله لنا ولكم، أنتم سلفنا ونحن على الاثر
”Amani iwe juu yenu, enyi watu wa makaburi. Allaah atusamehe sisi na nyinyi. Nyinyi ndio watangulizi wetu na sisi tuko nyuma yenu.”
Ameipokea at-Tirmidhiy (2/156) na adh-Dhwiyaa´ katika ”al-Mukhtaarah” (58/192/1) kwa njia ya at-Twabaraaniy. at-Tirmidhiy amesema: ”Ni nzuri na ngeni.”
Katika cheni yake ya wapokezi yupo Qaabuus bin Abiy Dhwibyaan. an-Nasaa’iy amesema: ”Si mwenye nguvu.” Ibn Hibbaan amesema: ”Kumbukumbu yake ni mbaya. Anapokea peke yake kutoka kwa baba yake kwa mambo yasiyo na msingi.”
Haya ni katika mapokezi yake kutoka kwa baba yake. Kwa hivyo haifai kutegemewa. Huenda at-Tirmidhiy kuizingatia kuwa nzuri ni kutokana na nyenginezo zinazoipa nguvu, kwa kuwa maana yake imethibiti katika Hadiyth Swahiyh. Sehemu nzuri ya hizo imekwishatajwa hivi karibuni. Lakini maneno yake:
”… akawakabili kwa uso wake.”
ni dhaifu na inayopingana na Hadiyth zilizo Swahiyh kwa kuwa huyu mwenye mapokezi haya ndiye pekee aliyepokea hivyo. Ukishajua hili, basi Shaykh ´Aliy al-Qaariy amesema katika ”Mirqaat-ul-Mafaatiyh” (2/407):
“Ndani yake kuna dalili kwamba kinachopendeza wakati wa kuwasalimia maiti ni kuelekea uso wa maiti na aendelee hivyo hivyo wakati wa kuomba du´aa. Hivyo ndivyo walivyofanya waislamu kwa ujumla, kinyume na alivyosema Ibn Hajar kuwa Sunnah kwetu ni kwamba wakati wa kuomba du´aa aelekee Qiblah, kama ilivyofahamika kutokana na Hadiyth nyingine kuhusu kuomba du´aa kwa ujumla.”
Katika kujengea hoja huku kuna dosari ya wazi, kwa sababu ndani ya Hadiyth hakuna isipokuwa yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuuelekeza uso wake kuyaelekea makaburi. Kuhusu kuuelekea uso wa maiti, hilo ni jambo jingine ambalo linahitaji dalili ya wazi tofauti na hii, nayo ni jambo nisilolijua. Basi haki ni kwamba, lau Hadiyth hii cheni yake ya wapokezi imethibiti, basi ingelikuwa dalili iliyo wazi kuwa anayepita karibu na makaburi huwageuzia uso wake wakati wa kuwasalimia na kuwaombea du´aa, bila kujali kama anakabili uso wa maiti au hapana, bali kwa namna tu aliyekuwepo – kwa kadiri hali inavyowezesha – bila ya nia ya makusudi ya kuuelekea uso wa maiti. Ama kwa kuwa cheni ya wapokezi ni dhaifu, kama ilivyobainishwa, basi haifai kabisa kuijengea hoja. Hili halipingani na yale yaliyotangulia kutoka kwa Imaam Maalik kuhusu kutosuniwa kulielekea kaburi wakati wa kuomba du´aa. Hii ni kinyume na simulizi inayodai kuwa Maalik alipoulizwa na al-Mansuur al-‘Abbaasiy kuhusu kulielekea kaburi, alimwamrisha afanye hivyo na akasema:
”Hiyo ni njia yako na njia ya baba yako Aadam.”
Hii ni simulizi batili na ya uongo juu ya Maalik. Haina mlolongo wa wapokezi unaotambulika. Pia inakwenda kinyume na yaliyothibiti kutoka kwake kwa njia za kutegemewa katika vitabu vya wanafunzi wake, kama alivyosema Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Qaadhwiy na wengine. Mfano wake ni simulizi nyingine waliyopokea kutoka kwake kwamba aliulizwa kuhusu watu wanaosimama muda mrefu wakielielekea kaburi hali ya kujiombea wao wenyewe du´aa, basi Maalik akakemea kitendo hicho na akasema:
”Hayo ni miongoni mwa Bid´ah ambazo hazikufanywa na Maswahabah na wale walowafuata kwa wema.”
Amesema tena:
”Hautofaulu mwisho wa ummah huu isipokuwa kwa yale yaliyowafanya kufaulu wa mwanzo wao.”[4]
[1] 40:60
[2] Alifariki mwaka wa 17. Wasifu wake umeandikwa katika ”Tadhkirat-ul-Huffaadhw” (04/126) ya adh-Dhahabiy.
[3] Ama yale aliyopokea ´Ismaa´iyl al-Qaadhwiy katika ”Fadhwl-is-Swalaati ´alaan-Nabiy (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)”, na. 101 kwa ukaguzi wangu na chapa ya Maktabah al-Islaamiy, kutoka kwa Ibn ´Umar ambaye amesimulia:
”Ya kwamba alikuwa akimwendea (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiweka mkono wake juu ya kaburi lake, akielekea Qiblah kisha anamsalimia.”
ni dhaifu na inayopingana na Hadiyth zilizo Swahiyh, kama nilivyobainisha wakati nilipoitolea maelezo.
[4] Tazama ”al-Qaa´idah al-Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah”, uk. 53-62.
- Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 246-251
- Imechapishwa: 09/08/2026

Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 246-251
Imechapishwa: 09/08/2026
https://firqatunnajia.com/130-makatazo-ya-kuelekea-kaburi-wakati-wa-kumuombea-duaa-maiti/