120 – Inajuzu kuinua mikono wakati kumuombea du´aa maiti. Hilo ni kutokana na Hadiyth ya ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) aliposema:
”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) usiku mmoja alitoka, nikamtuma Bariyrah nyuma yake aone alikoenda. Akasema: ”Alielekea upande wa Baqiy´ al-Gharqad, akasimama sehemu ya chini ya Baqiy´ kisha akainua mikono yake, kisha akaondoka. Bariyrah akarudi kwangu na kunijulisha. Asubuhi ilipopambazuka nikamuuliza: ”Ee Mtume wa Allaah, umetoka wapi usiku wa jana?” Akasema: ”Nilitumwa kwa watu wa Baqiy´ ili niwaombee du´aa.”
Ameipokea Ahmad (6/92), na imo katika ”al-Muwattwa´” (1/239-240), na kutoka humo an-Nasaa´iy (1/287) amepokea mfano wake, isipokuwa hakujatajwa ndani yake kuinua mikono. Cheni yake ya wapokezi ni nzuri.
Kuinua mikono kumethibiti katika kisa kingine cha ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) kilichotangulia katika masuala ya 119.
- Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 246
- Imechapishwa: 09/08/2026
120 – Inajuzu kuinua mikono wakati kumuombea du´aa maiti. Hilo ni kutokana na Hadiyth ya ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) aliposema:
”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) usiku mmoja alitoka, nikamtuma Bariyrah nyuma yake aone alikoenda. Akasema: ”Alielekea upande wa Baqiy´ al-Gharqad, akasimama sehemu ya chini ya Baqiy´ kisha akainua mikono yake, kisha akaondoka. Bariyrah akarudi kwangu na kunijulisha. Asubuhi ilipopambazuka nikamuuliza: ”Ee Mtume wa Allaah, umetoka wapi usiku wa jana?” Akasema: ”Nilitumwa kwa watu wa Baqiy´ ili niwaombee du´aa.”
Ameipokea Ahmad (6/92), na imo katika ”al-Muwattwa´” (1/239-240), na kutoka humo an-Nasaa´iy (1/287) amepokea mfano wake, isipokuwa hakujatajwa ndani yake kuinua mikono. Cheni yake ya wapokezi ni nzuri.
Kuinua mikono kumethibiti katika kisa kingine cha ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) kilichotangulia katika masuala ya 119.
Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 246
Imechapishwa: 09/08/2026
https://firqatunnajia.com/129-kufaa-kunyanyua-mikono-wakati-wa-kumuombea-duaa-maiti-makaburini/