Kuhusu yale yaliyotajwa katika kitabu ”ar-Ruuh” cha Ibn-ul-Qayyim, uk. 13:
”al-Hallaal amesema: al-Hasan bin Ahmad al-Warraaq amenikhabarisha: ‘Aliy bin Muusa al-Haddaad ametuhadithia – ambaye alikuwa mkweli – amesema: ”Nilikuwa pamoja na Ahmad bin Hanbal na Muhammad bin Qudaamah al-Jawhariy katika jeneza. Basi walipomzika maiti, alikaa mtu kipofu akisoma juu ya kaburi, ndipo Ahmad akamwambia: “Ee mtu! Hakika kusoma juu ya kaburi ni Bid‘ah!” Nilipotoka makaburini, Muhammad bin Qudaamah akamwambia Ahmad bin Hanbal: “Ee Abu ‘Abdillaah! Unasemaje kuhusu Mubashshir al-Halabiy?” Akasema: “Ni mtu mwaminifu.” Akasema: “Je, umeandika kutoka kwake chochote?” Akasema: “Ndio.” Akasema: ” Mubashshir kutoka kwa ´Abdur-Rahmaan bin al-‘Alaa´ bin al-Lajlaaj akanikhabarisha (asili ni: al-Hallaaj na hilo ni kosa), kutoka kwa baba yake kwamba aliusia pindi atakapozikwa basi asomewe kichwani mwake sehemu ya mwanzoni na ya mwishoni mwa al-Baqarah na akasema kwamba amemsikia Ibn ‘Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) akiusia jambo hilo.” Basi Ahmad akamwambia: “Rudi ukamwambie mtu yule asome.”
Majibu ya jambo hili yako kwa njia kadhaa:
1 – Kuna mashaka kuhusu kusihi kwa kisa hiki kutoka kwa Ahmad, kwa kuwa Shaykh wa al-Hallaal al-Hasan bin Ahmad al-Warraaq sikupata wasifu wake katika vitabu nilivyo navyo sasa vya wasimulizi. Vivyo hivyo Shaykh wake ‘Aliy bin Muusa al-Haddaad sikumtambua. Hata kama imeelezwa kuwa ni “mwaminifu”, inaonekana kuwa msemaji wa hilo ni huyu al-Warraaq mwenyewe, na tayari umeshaielewa hali yake.
2 – Hata kama kisa hicho kimesihi, basi ni maalum zaidi kuliko yaliyopokewa na Abu Daawud kutoka kwake. Kwa kuunganisha riwaya mbili hizi kutoka kwake inapatikana kuwa msimamo wake ni kuchukia kusoma Qur-aan makaburini isipokuwa wakati wa mazishi tu.
3 – Cheni ya wapokezi ya masimulizi haya haitambuliki kwa Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) hata kama tutakubali kuwa imesihi kutoka kwa Ahmad, kwa kuwa ´Abdur-Rahmaan bin al-‘Alaa’ bin al-Lajlaaj ni miongoni mwa wasiojulikana, kama linavyoashiria hilo na maneno ya adh-Dhahabiy katika wasifu wake katika ”al-Miyzaan”:
“Hakuna aliyepokea kutoka kwake isipokuwa huyu Mubashshir.”
Kwa njia yake amepokea Ibn ‘Asaakir (13/399/2).
Ama kitendo cha Ibn Hibbaan kumzingatia kuwa ni mwenye kuaminika hakitegemewi kutokana na vile anavyotambulika kuchukulia wepesi kuwafanya wasimulizi ni wenye kuaminika, kwa sababu hiyo Haafidhw hakulizingatia hilo katika ”at-Taqriyb” aliposema kuhusu mtu huyo:
“Mwenye kukubaliwa.”
Kwa maana anapoungwa mkono tu, lakini akiwa peke yake basi Hadiyth yake ni dhaifu, kama alivyoeleza katika ”Muqaddimah” yake. Kinachotilia nguvu jambo hilo ni kwamba at-Tirmidhiy, licha kuchukulia kwake wepesi katika kuzifanya Hadiyth kuwa nzuri, alipotoa Hadiyth nyingine kutoka kwake (2/128), hakuipa hata sifa ya kuwa nzuri.
4 – Kwamba lau ingethibiti cheni ya wapokezi wake kutoka kwa Ibn ´Umar, basi ni kama masimulizi ya Swahabah na si yenye kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa hivyo hakuna hoja kabisa. Mfano wa masimulizi haya ni yale aliyotaja Ibn-ul-Qayyim, uk. 14:
”al-Hallaal ametaja kutoka kwa ash-Sha´biy kwamba amesema: ”Answaar walikuwa wanapofiwa na maiti basi wanaelekea kaburini kwake wakisoma Qur-aan.”
Basi sisi tuna shaka kuhusu kuthibiti kwake kutoka kwa ash-Sha´biy na khaswa kwa tamko hili, kwani nimemuona as-Suyuutwiy ameitaja katika ”Sharh-us-Swuduur”, uk. 15 kwa tamko lisemalo:
”Answaar walikuwa wakisoma mbele ya maiti Suurah ”al-Baqarah.”
Akasema: ”Ameipokea Ibn Abiy Shaybah na al-Marwaziy. Ameitaja katika ”Mlango unaozungumzia yale anayotakiwa kusema mtu katika maradhi ya mauti na kinachosomwa mbele yake.”
Kisha nikamuona katika ”al-Muswannaf” ya Ibn Abiy Shaybah (4/74) na akaiwekea kichwa cha khabari kinachosema ”Mlango wa kinachosemwa kwa mgonjwa anapotaka kukata roho.”
Basi ikabainika ya kwamba katika cheni ya wapokezi wake yupo Mujaalid, ambaye ni Ibn Sa´iyd. Haafidhw amesema katika ”at-Taqriyb”:
”Si mwenye nguvu na alibadilika mwishoni mwa umri wake.”
Hivyo basi ikaonekana wazi kuwa masimulizi haya si kuhusu kusoma kwenye kaburi, bali ni wakati wa kukata roho. Tukiachia mbali kwamba cheni ya wapokezi wake ni dhaifu.
Kuhusu Hadiyth isemayo:
”Anayepita makaburini kisha akasoma ”Qul huwa Allaahu Ahad” mara kumi na moja kisha akawagawia thawabu zake wafu, basi atapewa thawabu kwa idadi ya wafu.”
ni Hadiyth batili na iliyotungwa. Ameipokea Abu Muhammad al-Hallaal katika ”al-Qiraa-ah ´alal-Qubuur”, uk. (2/201) na ad-Daylamiy kutoka kwa nakala ya ´Abdullaah bin Ahmad bin ´Aamir, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa ´Aliy ar-Ridhwaa, kutoka kwa mababu zake, nayo ni nakala ya kuzuliwa na batili isiyoepukana na uzushi wa ´Abdullaah huyu au uzushi wa baba yake, kama alivyosema adh-Dhahabiy katika ”al-Miyzaan” na akaungwa mkono na Haafidhw Ibn Hajar katika ”al-Lisaan”, kisha as-Suyuutwiy katika ”Dhayl-ul-Ahaadiyth al-Mawdhwuu´ah” na akailetea Hadiyth hii na akamfuata Ibn ´Iraaq katika ”Tanziyh-ush-Shariy´ah al-Marfuu´ah ´anil-Ahaadiyth ash-Shiy´ah al-Mawdhwuu´ah”. Kisha as-Suyuutwiy akasahau kuhusu hilo akaitaja Hadiyth hii katika ”Sharh-us-Swuduur”, uk. 130 kwa mapokezi ya Abu Muhammad as-Samarqandiy katika ”Fadhwaa-il Qul huwa Allaahu Ahad” na akainyamazia. Ndio, hakika alikuwa ameshatilia ishara kabla ya hapo kuhusu udhaifu wake, lakini hilo halitoshi, kwani Hadiyth ni ya kutungwa kwa kukiri kwake. Kwa hivyo haitoshi kuidhoofisha tu, kama ambavyo haifai kuinyamazia, kama alivyofanya Shaykh Ismaa´iyl al-´Ajaluwniy katika ”Kashf-ul-Khafaa´” (2/382), kwani ameinasibisha kwa ar-Raafi´iy katika ”Taariykh” yake na akainyamazia. Pamoja na kuwa ameweka kitabu chake kilichotajwa kwa ajili ya kufichua ”kilichoenea miongoni mwa Hadiyth kwa ndimi za watu”. Kisha kunyamaza kwa wataalamu kuhusu Hadiyth kunaweza kumdanganya asiyekuwa na elimu nayo kuwa Hadiyth ni miongoni mwa zile zinazofaa kutumiwa kama hoja au kuzifanyia kazi katika fadhilah za matendo, kama wanavyosema, hili ndilo lililotokea katika Hadiyth hii. Nimewaona baadhi ya Hanafiyyah wamejengea hoja Hadiyth hii kwa ajili ya kusoma Qur-aan kwenye makaburi, naye ni Shaykh at-Twahtwaawiy katika ”Maraaqiy-ul-Falaah”, uk. 117. Naye ameinasibisha kwa ad-Daaraqutwniy, jambo ambalo nadhani kuwa ni kosa kwa sababu sijamuona mwingine yeyote aliyeinasibisha kwake. Kisha lililo maarufu kwa wanaojishughulisha na elimu hii ni kwamba kuiegemeza kwa ad-Daaraqutwniy kwa ujumla kunakusudiwa kitabu chake ”as-Sunan” na Hadiyth hii sijaiona ndani yake – na Allaah ndiye mjuzi zaidi.
- Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 243-245
- Imechapishwa: 09/08/2026

Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 243-245
Imechapishwa: 09/08/2026
https://firqatunnajia.com/128-uchambuzi-wa-kielimu-kuhusu-masimulizi-yanayojuzisha-kusoma-qur-aan-kwenye-makaburi/