Swali: Wengi wa jamaa zangu kwa upande wa baba yangu aliyefariki na pia jamaa wa mke wangu wamezoea kuchanganyika wanaume na wanawake na wamefanya hilo kuwa ni desturi yao. Wanaume wanawasalimia wanawake kwa mikono na wanakaa pamoja nao. Kwa sababu hiyo siendi kwao pamoja na mke wangu kabisa. Nilijaribu kwenda peke yangu ili kudumisha uhusiano, lakini wanawake wao wakaanza kujaribu kunisalimia kwa mikono kwa kunichokoza kwa kuwa wanajua kuwa mimi sisalimiani kwa mikono na wanawake. Wakaanza kufanya mambo yanayonikera na matokeo yake nikaacha pia kuwatembelea. Sasa kuna karibu kuwa na kukatika kwa uhusiano baina yetu na ninaogopa nisiingie katika kundi la wanaokata uhusiano wa jamaa. Wakati huohuo siwezi kujua nifanye nini. Nifanye nini?
Jibu: Wewe si mkataji wa uhusiano, ee ndugu yangu, bali wao ndio wanaokata. Wewe si mkataji, wao ndio wanaokata. Mwenye kuendelea katika maovu, akashikamana nao na akakataa kuacha, huyo ndiye mkataji na si wewe. Ikiwa unaweza kuwapa nasaha bila ya kusalimiana na wanawake kwa mikono na bila ya kuwatazama wanawake waliojifunua, kwa kushusha chini macho yako na kutopeana mikono na kusema haki, basi fanya hivyo na jitahidi. Ikiwa huwezi, basi wewe ni mwenye kupewa udhuru. Wao ndio wanaokata na wewe si mkataji.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3305/حكم-مصافحة-النساء-الاجنبيات-والنظر-اليهن
- Imechapishwa: 08/08/2026
Swali: Wengi wa jamaa zangu kwa upande wa baba yangu aliyefariki na pia jamaa wa mke wangu wamezoea kuchanganyika wanaume na wanawake na wamefanya hilo kuwa ni desturi yao. Wanaume wanawasalimia wanawake kwa mikono na wanakaa pamoja nao. Kwa sababu hiyo siendi kwao pamoja na mke wangu kabisa. Nilijaribu kwenda peke yangu ili kudumisha uhusiano, lakini wanawake wao wakaanza kujaribu kunisalimia kwa mikono kwa kunichokoza kwa kuwa wanajua kuwa mimi sisalimiani kwa mikono na wanawake. Wakaanza kufanya mambo yanayonikera na matokeo yake nikaacha pia kuwatembelea. Sasa kuna karibu kuwa na kukatika kwa uhusiano baina yetu na ninaogopa nisiingie katika kundi la wanaokata uhusiano wa jamaa. Wakati huohuo siwezi kujua nifanye nini. Nifanye nini?
Jibu: Wewe si mkataji wa uhusiano, ee ndugu yangu, bali wao ndio wanaokata. Wewe si mkataji, wao ndio wanaokata. Mwenye kuendelea katika maovu, akashikamana nao na akakataa kuacha, huyo ndiye mkataji na si wewe. Ikiwa unaweza kuwapa nasaha bila ya kusalimiana na wanawake kwa mikono na bila ya kuwatazama wanawake waliojifunua, kwa kushusha chini macho yako na kutopeana mikono na kusema haki, basi fanya hivyo na jitahidi. Ikiwa huwezi, basi wewe ni mwenye kupewa udhuru. Wao ndio wanaokata na wewe si mkataji.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3305/حكم-مصافحة-النساء-الاجنبيات-والنظر-اليهن
Imechapishwa: 08/08/2026
https://firqatunnajia.com/ameacha-kuwatembelea-ndugu-wanaomsumbua-katika-dini-yake/