Anasubiri kutoa zakaah ya ardhi baada ya mauzo

Swali: Nimenunua kiwanja cha ardhi na kwa sasa nimekiweka kiuzwe, lakini sijatoa zakaah yake mpaka sasa kwa sababu nilikusudia nitalipa zakaah nitakapokiuza kwa miaka yote ambayo sikutoa zakaah.

Jibu: Ikiwa ardhi hiyo uliinunua kwa nia ya kuifanya biashara, basi ni wajibu utoe zakaah kila mwaka kulingana na thamani yake kwa mwaka huo, ni mamoja iwe imepanda bei au imeshuka. Kwa sababu miaka hutofautiana; wakati mwingine huwa nafuu na wakati mwingine huwa ghali. Hivyo basi unatakiwa kuitathmini kila mwaka kwa kushauriana na wataalamu wa thamani ya ardhi, kisha utoe zakaah kulingana na thamani itakayobainika kwa kila mwaka mpaka pale utakapoiuza.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3294/كيفية-زكاة-الارض-المعدة-للبيع
  • Imechapishwa: 08/08/2026