Swali: Je, du´aa ya imamu na maamuma kusema “Aamiyn” baada ya swalah ya faradhi ni katika Bid´ah? Je, inajuzu kuinua mikono katika dua ya Qunuut?
Jibu: Kuwa imamu anafanya du´aa baada ya swalah tano za faradhi na maamuma wanaitikia “Aamiyn”, hili ni Bid´ah na halina asili. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakulifanya na wala Maswahabah wake hawakulifanya. Imamu anapotoa salamu na maamuma pia, kila mmoja ashughulike na kumtaja Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Ama imamu kuinua mikono na kuomba du´aa na wengine kuitikia “Aamiyn”, hili halina msingi na ni katika Bid´ah.
Ama Qunuut, hilo ni jambo lililowekwa katika Shari´ah na kuinua mikono katika Qunuut ni jambo limesuniwa. Imethibiti kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiinua mikono yake katika Qunuut wakati wa misiba na Qunuut ya witr ni kama hiyo, sawa na Qunuut ya majanga.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3304/حكم-الدعاء-بعد-الفريضة-ورفع-اليدين-في-القنوت
- Imechapishwa: 08/08/2026
Swali: Je, du´aa ya imamu na maamuma kusema “Aamiyn” baada ya swalah ya faradhi ni katika Bid´ah? Je, inajuzu kuinua mikono katika dua ya Qunuut?
Jibu: Kuwa imamu anafanya du´aa baada ya swalah tano za faradhi na maamuma wanaitikia “Aamiyn”, hili ni Bid´ah na halina asili. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakulifanya na wala Maswahabah wake hawakulifanya. Imamu anapotoa salamu na maamuma pia, kila mmoja ashughulike na kumtaja Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Ama imamu kuinua mikono na kuomba du´aa na wengine kuitikia “Aamiyn”, hili halina msingi na ni katika Bid´ah.
Ama Qunuut, hilo ni jambo lililowekwa katika Shari´ah na kuinua mikono katika Qunuut ni jambo limesuniwa. Imethibiti kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiinua mikono yake katika Qunuut wakati wa misiba na Qunuut ya witr ni kama hiyo, sawa na Qunuut ya majanga.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3304/حكم-الدعاء-بعد-الفريضة-ورفع-اليدين-في-القنوت
Imechapishwa: 08/08/2026
https://firqatunnajia.com/duaa-za-pamoja-baada-ya-swalah-za-faradhi-ni-bidah/