Swali: Je, ni bora kwa wanawake kuswali swalah ya mkusanyiko ikiwa wapo katika nyumba moja? Je, imamu wao awasikilizishe sauti yake?
Jibu: Hili ni jambo bora zaidi iwapo itawezekana waswali swalah ya mkusanyiko katika nyumba yao na awaswalishe yule aliye mbele yao kwa elimu na fadhilah. Hili huwa zuri zaidi, kwa sababu linapatikana faida ya kufundishana, kuiga katika utulivu wa swalah na kusikia kisomo. Atawasikiza sauti yake katika swalah za kusoma kwa sauti, kama vile Maghrib, ´Ishaa na Fajr. Katika hili kuna kheri. Imepokewa kutoka kwa ‘Aaishah na Umm Salamah (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ya kwamba walikuwa wakiwaongoza wanawake swalah nyumbani mwao nyakati fulani.
Kwa kumalizia ni kwamba hapana shida wanawake kuwaswalisha wanawake wenzake katika swalah ya mkusanyiko nyumbani. Ni jambo zuri na linaweza kunufaisha sana, khaswa ikiwa imamu ni miongoni mwa wenye elimu na uelewa ambapo anawaelekeza na anawaswalisha swalah ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa utulivu, bila haraka na bila Bid´ah. Vilevile anawafundisha na kuwaongoza baada ya swalah na katika nyakati nyingine. Yote hayo ni mambo mazuri.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1486/حكم-صلاة-النساء-جماعة-في-البيت
- Imechapishwa: 21/12/2025
Swali: Je, ni bora kwa wanawake kuswali swalah ya mkusanyiko ikiwa wapo katika nyumba moja? Je, imamu wao awasikilizishe sauti yake?
Jibu: Hili ni jambo bora zaidi iwapo itawezekana waswali swalah ya mkusanyiko katika nyumba yao na awaswalishe yule aliye mbele yao kwa elimu na fadhilah. Hili huwa zuri zaidi, kwa sababu linapatikana faida ya kufundishana, kuiga katika utulivu wa swalah na kusikia kisomo. Atawasikiza sauti yake katika swalah za kusoma kwa sauti, kama vile Maghrib, ´Ishaa na Fajr. Katika hili kuna kheri. Imepokewa kutoka kwa ‘Aaishah na Umm Salamah (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ya kwamba walikuwa wakiwaongoza wanawake swalah nyumbani mwao nyakati fulani.
Kwa kumalizia ni kwamba hapana shida wanawake kuwaswalisha wanawake wenzake katika swalah ya mkusanyiko nyumbani. Ni jambo zuri na linaweza kunufaisha sana, khaswa ikiwa imamu ni miongoni mwa wenye elimu na uelewa ambapo anawaelekeza na anawaswalisha swalah ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa utulivu, bila haraka na bila Bid´ah. Vilevile anawafundisha na kuwaongoza baada ya swalah na katika nyakati nyingine. Yote hayo ni mambo mazuri.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1486/حكم-صلاة-النساء-جماعة-في-البيت
Imechapishwa: 21/12/2025
https://firqatunnajia.com/swalah-ya-mkusanyiko-kwa-wanawake-wanaoishi-nyumba-moja/