Anayesujudu sijda ya shukurani ya Suurah Swaad ndani ya swalah

Swali: Baadhi ya wanazuoni wamesema kuwa sujuud ya Suurah ”Swaad” ni sijda ya shukurani na hivyo inasujudiwa nje ya swalah na akifanya hivo ndani ya swalah basi swalah yake hubatilika. Je, hilo ni sahihi?

Jibu: Ndiyo, sijda ya ”Swaad” ni sijda ya kushukuru na hapana shaka juu ya hilo. Lakini anayefautisha kati ya ndani ya swalah na nje ya swalah, maneno yake si sahihi. Bali lililo sahihi ni kwamba hufanywa ndani ya swalah na nje ya swalah. Anayesema haifanywi ndani ya swalah basi amekosea. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliswali kwa Suurah ”Swaad” na akasujudu humo na alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) juu ya mimbari. Kwa hiyo anayesoma Suurah hiyo Sunnah ni kusujudu, ni mamoja awe yuko ndani ya swalah ya faradhi na Tarawiyh au awe nje ya swalah. Sunnah kwake ni kusujudu kwa hali zote, hata akiwa ndani ya swalah. Kwa hiyo anayesema kuwa sijda hiyo inabatilisha swalah, basi hayo ni maneno ya kimakosa na hayana msingi wowote katika Shari´ah kabisa.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1490/حكم-سجدة-سورة-ص-في-الصلاة-وخارجها
  • Imechapishwa: 21/12/2025