Swalah ya mamkuzi ya msikiti kwa aliyetoka kwa ajili ya kutawadha

Swali: Wakati tumekaa msikitini inatokea wakati mwingine anatoka nje mmoja wetu ili atawadhe kisha anarejea msikitini. Je, aswali swalah ya mamkuzi ya msikiti?

Jibu: Ndio, aswali swalah ya mamkuzi ya msikiti na aswali Sunnah ya wudhuu´ pia. Mtu ambaye atakariri kuingia mara nyingi basi aswali ile mara ya mwisho. Akitoka nje mara moja kwa ajili ya kutawadha basi aswali. Pia inafaa kwake kukusanya kati ya Sunnah mbili hizo; swalah ya mamkuzi ya msikiti na swalah ya Sunnah ya wudhuu´.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (22)
  • Imechapishwa: 18/09/2021