Swalah ya maamuma inaharibika kwa kuharibika swalah ya imamu?

Swali: Je, swalah ya maamuma inaharibika kwa kuharibika swalah ya imamu?

Jibu: Hapana. Swalah ya maamuma ni sahihi. Msingi ni kubaki kusiki kwa swalah na haibatiliki isipokuwa kwa dalili sahihi. Imamu imebatilika swalah yake kutokana na dalili sahihi, lakini maamuma amejiunga na amri ya Allaah na kwa ajili hiyo swalah yake haiwezi kuharibika isipokuwa kwa amri ya Allaah. Kinachovuliwa katika hali hiyo ni yale yanayochukua nafasi ya maamuma kama mfano wa Sutrah. Sutrah ya imamu ndio Sutrah ya wale walio nyuma yake. Anapopita mwanamke kati ya imamu na Sutrah yake, basi inabatilika swalah ya imamu na ya maamuma zote pamoja. Kwa sababu Sutrah hizi ni zenye kushirikiana. Kwa ajili hii hatumwamrishi maamuma kuweka Sutrah. Bali akijiwekea Sutrah atazingatiwa ni mwenye kujikalifisha na mzushi.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/450-451)
  • Imechapishwa: 17/04/2026