Swali: Mtu amepitiwa na usingizi na akapitwa na Fajr. Ni lini atailipa?

Jibu: Atailipa pale tu atapokumbuka. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule mwenye kupitikiwa na usingizi au akaisahau swalah, basi aiswali pale atapoikumbuka. Haina kafara nyingine isipokuwa hiyo.”[1]

Ina maana kwamba ataikidhi pale tu atapokumbuka na pale atapoamka. Msingi katika amri ni uwajibu na uharaka. Ikiwa mtu atauliza ni kwa nini Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwaamrisha Maswahabah kutoka yale maeneo waliyopitiwa na usingizi wakakosa Fajr na kwenda mahali pengine, jawabu ni kwamba alitoa sababu kwamba sehemu hiyo alipohudhuria shaytwaan[2]. Haitakikani kuswali maeneo ambayo wamehudhuria mashaytwaan.

[1] al-Bukhaariy (597) na Muslim (684).

[2] Muslim (680).

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/219-220)
  • Imechapishwa: 17/04/2026