Msafiri amejiunga na imamu mkazi katika zile Rak´ah mbili za mwisho

Swali: Msafiri amejiunga na imamu mkazi katika zile Rak´ah mbili za mwisho. Je, atoe salamu pamoja naye kwa nia ya kufupisha?

Jibu: Haijuzu kwa msafiri anaposwalishwa na imamu mkazi kufupisha swalah. Dalili ya hilo ni ueneaji wa maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Kile mnachowahi swalini, na kile kilichokupiteni kamilisheni.”[1]

Kutokana na hili pindi msafiri anapojiunga na imamu mkazi katika zile Rak´ah mbili za mwisho, basi ni wajibu kwake kuswali Rak´ah zingine mbili baada ya Tasliym ya imamu. Haijuzu kwake kutoa salamu pamoja na imamu na kutosheka na zile Rak´ah mbili alizoswali – na Allaah ndiye mjuzi zaidi.

[1] al-Bukhaariy (636) na Muslim (602).

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/452)
  • Imechapishwa: 17/04/2026