Amesahau kusema kwamba swalah ni bora kuliko usingizi

Swali: Muadhini amesahau kusema:

الصلاة خير من النوم

“Swalah ni bora kuliko usingizi.”

Kipi kinachomlazimu?

Jibu: Muadhini akisahau kusema:

الصلاة خير من النوم

“Swalah ni bora kuliko usingizi.”,

kinachotambulika kati ya wanazuoni ni kwamba adhaana yake ni sahihi. Kwa sababu jumla hiyo inapendeza tu na si kwamba ni lazima. Ni bora kuisema baada ya kupambazuka, endapo ataiacha hapana vibaya.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/188)
  • Imechapishwa: 17/04/2026