Swalah ya kupatwa kwa jua inaswaliwa mara moja na haikaririwi

Swali: Inachukiza iwapo atamaliza kuswali lakini bado jua limeendelea kupatwa kisha akaswali swalah nyingine?

Jibu: Hapana. Sunnah [ni mara moja na] inatosha. Awashughulishe watu na Dhikr, Takbiyr na swadaqah.

Swali: Vipi ikiwa mtu hakuwahi Rak´ah ya kwanza?

Jibu: Aikidhi. Ikiwa amewahi Rak´ah ya pili pekee basi ailipe ile Rak´ah ya kwanza. Kwa maana ya kwamba imamu anapotoa salamu akidhi ile Rak´ah ya kwanza kwa Rukuu´ mbili, Sujuud mbili na visomo viwili.

Swali: Akidhi yale yaliyompita au Rak´ah mbili?

Jibu: Aswali ile Rak´ah iliyompita kwa kisomo chake, Rukuu´ yake na Sujuud yake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23754/حكم-تكرار-صلاة-الكسوف-وقضاىها
  • Imechapishwa: 20/04/2024