Swalah ya jeneza msikitini au makaburini?

Swali: Bora ni kumswalia maiti makaburini au ni bora zaidi msikitini?

Jibu: Ni bora kuswali katika uwanja wa kuswalia au msikitini. Lakini haja ikipelekea kuswali makaburini, hapana ubaya. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliswalia jeneza makaburini. Hata hivyo bora zaidi ni kuswali uwanjani au msikitini ili watu waweze kukusanyika kwa wingi.

Swali: Vipi msikitini?

Jibu: Msikitini au katika uwanja wa kuswalia, kote ni kuzuri.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24825/هل-صلاة-الجنازة-في-المقبرة-افضل-ام-المسجد
  • Imechapishwa: 20/12/2024