Swali: Leo kumetokea jeneza kabla ya swalah ya Tarawiyh. Ni lipi bora kuliandama jeneza au tuswali swalah ya Tarawiyh? Ni lipi bora upande wa imamu acheleweshe swalah ya jeneza mpaka baada ya Tarawiyh au aliharakishe?
Jibu: Kumegongana hivi sasa mambo mawili na yote mawili yana ubora; kuliandama jeneza na Tarawiyh. Je, tulifuate jeneza na kuacha Tarawiyh au kinyume chake? Tutazame! Tarawiyh lau mtu ataiacha basi hakuna kitachompita isipokuwa tu swalah ya mkusanyiko. Kwa sababu anaweza kuswali Tahajjud nyumbani kwake. Ana wakati kuanzia wakati wa swalah ya ´Ishaa mpaka wakati wa kupambazuka kwa Fajr. Kuhusu jeneza iwapo itampita basi hiyo imekwishapita. Kujengea juu ya haya tunatakiwa kutanguliza jeneza. Lakini akichelea kwamba iwapo ataliandama jeneza basi atahisi uvivu na hivyo Tahajjud itampita, basi abaki. Isipokuwa ikiwa kama amelazimika kuliandama jeneza kwa njia ya kwamba hakuna ambao wanaweza kukidhi uwajibu wa kutosheleza. Katika hali hii aliandame jeneza.
- Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (71) http://binothaimeen.net/content/1622
- Imechapishwa: 23/03/2020
Swali: Leo kumetokea jeneza kabla ya swalah ya Tarawiyh. Ni lipi bora kuliandama jeneza au tuswali swalah ya Tarawiyh? Ni lipi bora upande wa imamu acheleweshe swalah ya jeneza mpaka baada ya Tarawiyh au aliharakishe?
Jibu: Kumegongana hivi sasa mambo mawili na yote mawili yana ubora; kuliandama jeneza na Tarawiyh. Je, tulifuate jeneza na kuacha Tarawiyh au kinyume chake? Tutazame! Tarawiyh lau mtu ataiacha basi hakuna kitachompita isipokuwa tu swalah ya mkusanyiko. Kwa sababu anaweza kuswali Tahajjud nyumbani kwake. Ana wakati kuanzia wakati wa swalah ya ´Ishaa mpaka wakati wa kupambazuka kwa Fajr. Kuhusu jeneza iwapo itampita basi hiyo imekwishapita. Kujengea juu ya haya tunatakiwa kutanguliza jeneza. Lakini akichelea kwamba iwapo ataliandama jeneza basi atahisi uvivu na hivyo Tahajjud itampita, basi abaki. Isipokuwa ikiwa kama amelazimika kuliandama jeneza kwa njia ya kwamba hakuna ambao wanaweza kukidhi uwajibu wa kutosheleza. Katika hali hii aliandame jeneza.
Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (71) http://binothaimeen.net/content/1622
Imechapishwa: 23/03/2020
https://firqatunnajia.com/swalah-ya-jeneza-kwanza-au-tarawiyh/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)