Swali 744: Mwanamume amemsusa mke wake kwa muda wa miaka miwili, hakumrejea kwa sababu ya watoto wake na wala hakusimamia wajibu wa matumizi. Mwanamke huyu hana ndugu wa kumhudumia. Hali yake ni ngumu sana. Amekatwa na kila mmoja isipokuwa Allaah peke yake. Shari´ah inasemaje juu ya mume kama huyu ambaye amemwacha mke wake? Mama wa watoto wake anasubiri hali hii mbaya yenye kuumiza.

Jibu: Hapana shaka kwamba mke ana haki ambazo zinamlazimu mume wake kuzitimiza. Amesema (Ta´ala):

وَلَهُنَّ مِثْلُ الَّذِي عَلَيْهِنَّ بِالْمَعْرُوفِ

“Nao wake wana haki kama ambayo [ya waume zao] iliyo juu yao kwa mujibu wa wema.”[1]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Wake zenu juu yenu wana haki.”

Allaah (Ta´ala) amesema:

فَإِمْسَاكٌ بِمَعْرُوفٍ أَوْ تَسْرِيحٌ بِإِحْسَانٍ

“Hivyo kuzuia kwa mujibu wa Shari´ah au kuachia kwa  wema.”

Zipo dalili zengine nyingi ambazo zinafahamisha kuwa ni lazima kwa mume kumcha Allaah (Ta´ala) juu ya mke wake na amtekeleze haki zake. Haijuzu akapunguza chochote katika haki zake isipokuwa kwa vigezo vya Kishari´ah. Moja katika vigezi hivo ni kama mke atakuwa mwasi.

[1] 02:228

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Mar´ah al-Muslimah, uk. 290
  • Imechapishwa: 23/03/2020