Swali: Swalah ya ´iyd ni faradhi mpaka kwa wanawake?

Jibu: Wanawake hapana sio faradhi. Lakini Abul-´Abbaas Ibn Taymiyyah amesema kuwa inaweza kusemwa kuwa ni wajibu kwao. Kinachotambulika kwa wanazuoni ni kwamba sio faradhi, inapendeza pale ambapo itawepesika kwao pasi na fitina.

Swali: Kwa wanaume ni faradhi kwa kila mmoja?

Jibu: Kinachotambulika ni kwamba ni faradhi kwa watu wote. Hivo ndivo anavoona Abu Haniyfah, chaguo la Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah, moja katika maoni ya Ahmad ni kwamba ni faradhi kwa kila mmoja kama ilivyo swalah ya ijumaa. Kilichoshuhurika kwa wanazuoni ni kwamba inapendeza. Wengine wakasema kuwa ni faradhi kwa baadhi ya watu. Kwa hivyo kuna maoni matatu. Ingawa maoni yanayosema kuwa ni lazima yana nguvu zaidi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23492/حكم-صلاة-العيد-للرجال-والنساء
  • Imechapishwa: 28/01/2024