Swali: Ni ipi hukumu ya kuswali nyuma ya imamu na Khatwiyb wa msikiti ambaye anafanya liwati na baada ya kuongea naye akasema kuwa ametubia licha ya kwamba bado tunatilia shaka tawbah yake?
Jibu: Bora aondolewe katika uimamu na tawbah yake ni yake mwenyewe. Tunamuomba Allaah amsamehe na amuwafikishe kutubia. Vinginevyo mafusaki hawastahiki kuwa maimamu. Allaah (´Azza wa Jall):
لَا يَنَالُ عَهْدِي الظَّالِمِينَ
”Haiwafikii Ahadi Yangu madhalimu.”[1]
Kwa vile bado ni muislamu inasihi kuswali nyuma yake. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Wawaongozeni katika swalah; wakipatia, basi mmepatia nyinyi na wao wamepatia; na wakikosea, basi nyinyi mmepatia na itakuwa dhidi yao.”
Lakini kazi ya uimamu ni heshima na wakati mnaposwali nyuma yake ni kama kwamba mnakubaliana na maovu anayofanya. Kama mnaweza kumwondosha, basi fanyeni hivo, na kama mnaweza kwenda katika msikiti mwingine, basi fanyeni hivo, na kama mnaweza kujitengenezea msikiti ijapo wa mbao, basi fanyeni hivo na baada ya kuyafanya hayo msiswali tena nyuma yake. Kuhusu kuswali nyuma yake hatuwezi kusema kuwa ni batili. Hata hivyo kufanyo hivo itakuwa ni kumuheshimisha. Kuhusu tawbah yake tunamuombea kwa Allaah amsamehe na awe ni mkweli katika jambo hilo.
[1] 02:124
- Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 314
- Imechapishwa: 13/07/2025
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket