Swali: Je, swalah ya ijumaa huanza baada ya kupinduka kwa jua?
Jibu: Inajuzu kuswali kabla ya kupinduka kwa jua. Hata hivyo lililo bora ni baada ya kupinduka kwa jua ili kutoka katika makinzano ya wanazuoni. Wanazuoni wengi wanasema kwamba ni lazima swalah ya ijumaa iwe baada ya kupondoka kwa jua. Haya ndio maoni ya jopo la wanazuoni. Wanazuoni wengine wameona kujuzu kabla ya kupinduka kwa jua katika saa ya sita. Kuna Hadiyth Swahiyh zinazoonyesha hilo. Wakiswali kabla ya kupinduka kwa jua kwa muda mfupi, basi swalah ni sahihi. Lakini inapasa icheleweshwe mpaka baada ya kupinduka kwa jua ili kutoka katika makinzano ya wanazuoni na kuwarahisishia watu ili wahudhurie wote na ili swalah iwe katika wakati mmoja. Hili ndilo lililo bora zaidi. Vinginevyo swalah inasihi hata kabla ya kupinduka kwa jua.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1592/هل-تجوز-صلاة-الجمعة-قبل-زوال-الشمس
- Imechapishwa: 27/06/2026
Swali: Je, swalah ya ijumaa huanza baada ya kupinduka kwa jua?
Jibu: Inajuzu kuswali kabla ya kupinduka kwa jua. Hata hivyo lililo bora ni baada ya kupinduka kwa jua ili kutoka katika makinzano ya wanazuoni. Wanazuoni wengi wanasema kwamba ni lazima swalah ya ijumaa iwe baada ya kupondoka kwa jua. Haya ndio maoni ya jopo la wanazuoni. Wanazuoni wengine wameona kujuzu kabla ya kupinduka kwa jua katika saa ya sita. Kuna Hadiyth Swahiyh zinazoonyesha hilo. Wakiswali kabla ya kupinduka kwa jua kwa muda mfupi, basi swalah ni sahihi. Lakini inapasa icheleweshwe mpaka baada ya kupinduka kwa jua ili kutoka katika makinzano ya wanazuoni na kuwarahisishia watu ili wahudhurie wote na ili swalah iwe katika wakati mmoja. Hili ndilo lililo bora zaidi. Vinginevyo swalah inasihi hata kabla ya kupinduka kwa jua.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1592/هل-تجوز-صلاة-الجمعة-قبل-زوال-الشمس
Imechapishwa: 27/06/2026
https://firqatunnajia.com/swalah-ya-ijumaa-kabla-ya-kupinduka-kwa-jua/