Ribaa inahusika katika vitu visivyo vya kuliwa wala dhahabu na fedha?

Swali: Je, ribaa huingia katika vitu visivyo vya kuliwa wala dhahabu na fedha, kama mfano wa mtu kuuza gari kwa magari mawili, kitabu kwa vitabu viwili au kondoo mmoja kwa kondoo wawili?

Jibu: Hapana, hili si katika ribaa. Ribaa iko katika vyakula vinavyopimwa kwa vipimo na kuhifadhiwa na katika vitu vinavyopimwa kwa mizani vinavyojulikana kwa kawaida. Ama kuuza gari kwa magari mawili, gari kwa ngamia, gari kwa nyumba au kwa ardhi, gari kwa kondoo au kondoo kwa ngamia, hakuna chochote, hapana vibaya kufanya hivo.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1604/جريان-الربا-في-غير-المكيلات-والموزونات
  • Imechapishwa: 27/06/2026