Swali: Wakati mwingine naswali nikiwa ninazuia upepo wa tumboni. Je, swalah yangu ni sahihi?

Jibu: Ni wajibu kwa muumini, ikiwa anasumbuliwa na upepo wa tumboni, mkojo au haja kubwa kwa namna inayomsumbua, asiingie katika swalah. Bali anatakiwa kwanza kujisaidia kwa haja kubwa au ndogo au kuutoa upepo wa tumboni, kisha atawadhe na aswali hali ya kuwa moyo wake na viungo vyake viko katika unyenyekevu na ameelekea katika swalah yake. Hili ndilo linalompasa kila muumini mwanamume na mwanamke. Hii ni kwa sababu ya maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Hakuna wakati chakula kishatengwa na wala wakati mtu anapozuiwa na mambo mawili machafu.”[1]

Maana ya mambo mawili machafu ni mkojo na haja kubwa na upepo wa tumboni unaingia katika maana yake. Kwa sababu upepo wa tumboni unapokuwa mkali unakuwa kama mkojo na haja kubwa katika kumdhuru anayeswali na kumshughulisha katika swalah yake. Hivyo kilichowekwa katika Shari´ah, ee dada kwa ajili ya Allaah, ni kwamba unapohisi upepo mkali wa tumboni ujitoe kwanza, kisha ufanye wudhuu´, halafu uswali.

[1] Muslim (560).

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (29/344)
  • Imechapishwa: 14/03/2026