Swali: Nilimuona mtu anayeswali Dhuhr makaburini ambapo nikamwambia kuwa swalah yake si sahihi. Je, maneno yangu haya ni sahihi?

Jibu: Ndio, ni sahihi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah awalaani mayahudi na manaswara, wameyafanya makaburi ya Mitume wao kuwa ni mahala pa kuswalia. Zindukeni! Msiyafanye makaburi kuwa ni mahali pa kuswalia. Hakika mimi nakukatazeni kufanya hivo.”

Haijuzu kuswali ndani ya makaburi. Mtu aswali nje yake. Kwa sababu kuswali makaburini ni miongoni mwa njia zinazopelekea katika shirki. Hivyo haisihi.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (22)
  • Imechapishwa: 25/09/2021