Swalah nyuma ya imamu unayemjua kuwa ni mshirikina

Swali: Baadhi ya watu wanaswali nyuma ya ambaye anafanya shirki kubwa na wanasema kuwa ni mjinga na kwamba ni muislamu. Ni ipi hukumu ya swalah hii?

Jibu: Akijua kuwa ni mshirikina ambaye anafanya shirki kubwa swalah yake haisihi nyuma yake. Haya ni kwa maafikiano ikiwa atatambua kuwa ni mshirikina. Ama akionelea kuwa bado ni muislamu swalah yake ni sahihi.

Swali: Ni ipi hukumu kuswali nyuma ya kuhani?

Jibu: Hakuswaliwi nyuma yake. Kwa sababu kuhani anaweza kuwa mshirikina. Anaweza kuwasadikisha wachawi, wanajimu na wengineo na matokeo yake akawa mfano wao.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 58-59
  • Imechapishwa: 02/07/2019