Mwanamke kupanda gari yeye na watoto wake na dereva wa kiume

Swali: Ni ipi hukumu ya mwanamke kupanda na dereva akiambatana na watoto wake wa kiume walio na umri kati ya miaka  tano, sita mpaka saba?

Jibu: Naona kuwa hili linatofautiana kidogo. Wapo baadhi ya madereva ambao ni waaminifu na hawawezi kuongea na wanawake sembuse kufanya naye mzaha au kumchekesha. Huyu huenda tukasema ambaye watoto wake wa kiume wamefikisha miaka hii ile faragha ya mwanaume na mwanamke iliokatazwa inaondoka. Laini dereva huyu [mwishoni] atafikia nini? Fatwa ninayotoa ni kukataza. Isipokuwa kama atakuwa na mwanaume ambaye kishabaleghe au mwanaume huyu [dereva] akawa pamoja na mwanamke katika Mahaarim zake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (51) http://binothaimeen.net/content/1165
  • Imechapishwa: 02/07/2019