Swali: Nikitawadha na nikakusudia kwa wudhuu´ wangu kuswali ´Aswr na nikaswali na nikabaki na twahara mpaka magharibi. Je, inafaa kuswali Maghrib kwa twahara ya swalah ya ´Aswr?
Jibu: Hakuna kikwazo cha kufanya hivo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliswali siku ya Ufunguzi wa Makkah swalah tano kwa wudhuu´ wa swalah ya Fajr kukiwemo Dhuhr na ´Aswr. Wakati ´Umar alipomuuliza akasema:
“Nimefanya kwa makusudi, ee ´Umar.”
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalish-Shaykh
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://www.mufti.af.org.sa/ar/content/هل-يجوز-الوضوء-الواحد-لكثر-من-صلاة
- Imechapishwa: 19/06/2022
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket