Swalah ndani ya chumba kilicho na picha au sanamu kinyago

Swali: Ni ipi hukumu ya kuswali ndani ya chumba ambacho mna picha au sanamu kinyago cha wanyama au mtu kwa ajili ya mapambo?

Jibu: Ni haramu kuhifadhi picha na masanamu vinyago na kuyaweka ndani ya nyumba. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Usiache picha isipokuwa umeiharibu wala kaburi lililoinuliwa isipokuwa umelisawazisha.”

Amesema vilevile (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Malaika hawaingii ndani ya nyumba ambayo ndani mna mbwa au picha.”

Inachukiza kuswali ndani ya chumba kilicho na picha iliyoning´inizwa au iliyosimikwa na khaswa ikiwa upande wa Qiblah cha mswaliji. Lakini hata hivo swalah ni sahihi.

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdur-Razzaaq ´Afiyfiy

´Abdullaah bin Ghudayyaan

Swaalih al-Fawzaan

´Abdul-´Aziyz Aalus-Shaykh

Bakr Abu Zayd

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Lajnah ad-Daaimah (16147)
  • Imechapishwa: 14/05/2022