Swalah na swawm kwa aliyepoteza fahamu kwa zaidi ya siku tatu

Swali: Je, kuweka mpaka wa siku tatu kumethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?

Jibu: Hapana, hili limepokelewa kutoka kwa ´Ammaar (Radhiya Allaahu ´anh) alipokuwa amepoteza fahamu. Vilevile kutoka kwa Samurah bin Jundub (Radhiya Allaahu ´anh) na kutoka kwa ´Imraan (Radhiya Allaahu ´anh). Hata hivyo sijapata cheni zake za wapokezi, ingawa yameelezwa kutoka kwao watatu hao. Mpaka sasa sijapata cheni zake za wapokezi, lakini ni maoni yaliyo karibu zaidi na usawa, kwa sababu siku tatu zimehusishwa na hukumu kadhaa. Kwa mfano wa haki ya kuchagua katika biashara ni siku tatu na mambo mengine mengi yameambatanishwa na siku tatu. Hivyo basi maoni hayo yako karibu na usahihi, kwa sababu usingizi unaweza kumshinda mtu, anaweza kulala siku moja, siku mbili au hata siku siku tatu.

Swali: Je, swawm pia inaingia humo ikiwa amepoteza fahamu zaidi ya siku tatu?

Jibu: Ndio, hana ulazima wa kulipa.

Swali: Vipi kuhusu waliotofautisha kati ya mwenye kupoteza fahamu na mwenye kulala – huyu amepoteza fahamu pasi na kutaka kwake mwenyewe na yule amelala kwa kutaka kwake mwenyewe – wapo sahihi?

Jibu: Hakuna shaka, lakini anafanana naye kwa kipindi cha siku tatu au chini yake, anafanana naye.

ar-Raajihiy: Ikiwa hakulipa swalah kwa sababu ya kupoteza fahamu ana haki zaidi ya kutolipiwa swawm pia?

Ibn Baaz: Hatolipiwa swawm wala swalah.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31540/هل-صح-تحديد-قضاء-الفواىت-بثلاثة-ايام
  • Imechapishwa: 03/11/2025