Swalah na swawm katika miji ya skandinavia

Swali: Katika baadhi ya miji aidha mchana au usiku unakuwa mrefu na wakati mwingine kunapita mwezi mzima ima inakuwa mchana tu au usiku. Mtu aswali vipi katika hali hii?

Jibu: Swalah katika hali hii inatakiwa kukadiriwa. Tatizo hili liliwahi kuletwa kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) baada ya kueleza kuwa pindi ad-Dajjaal atatumwa na kubaki katika ardhi siku arubaini ambapo siku moja itakuwa ni kama mwaka, siku ya nyingine itakuwa ni kama mwezi, siku nyingine itakuwa ni kama wiki na siku zilizobaki zitakuwa ni kawaida, ndipo Maswahabah wakamuuliza:

“Ee Mtume wa Allaah! Siku ambayo ni kama mwaka itatutosha kuswali swalah kama za siku moja?” Akawajibu: “Zikadirieni kiwango chake.”

Kwa msemo mwingine haitotosha kuswali kama swalah za siku moja. Tutaswali swalah za mwaka mzima ilihali ni siku moja. Hata hivyo itakuwa ni siku ndefu.

Kwa hivyo ile miji ambayo ima usiku au mchana unakuwa mrefu unazidi masaa ishirini na nne mtu anatakiwa kukadiria kiwango chake. Hivi sasa vipimo vipo na vinapatikana kwa urahisi. Mtu atakadiria kwa kutumia saa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (23)
  • Imechapishwa: 05/01/2019