Swali: Maneno ya baadhi ya wanazuoni kwamba mwenye kuacha swalah kwa makusudi hawezi kuilipa kutokana na maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Yeyote atakayefanya kitendo kisichoafikiana na amri yetu atarudishiwa mwenyewe.”[1]

Kwa hiyo mwenye kuacha kwa makusudi hatoiswali.

Jibu: Hilo ni ikiwa tutasema kwamba amekufuru, basi hatoilipa. Lakini tukisema kwamba hakufuru, basi atailipa kwa sababu yule mwenye kulala anatakiwa kuilipa atapoamka. Kwa hiyo yule aliyeiacha kwa makusudi ana haki zaidi ya kuilipa kwa mujibu wa maoni ya kikosi kikubwa cha wanazuoni.

Swali: Ijapo ataacha hata swalah moja tu?

Jibu: Maana ya Hadiyth ni ya yenye kuenea. Ikiwa ameiacha kwa makusudi mpaka muda wake ukaisha.

[1] Muslim (1718).

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31538/هل-يقضي-الصلاة-من-تركها-تعمدا
  • Imechapishwa: 01/11/2025