Suurah za Qur-aan nani alizipa majina?

Swali: Ni nani ambaye alizipa majina Suurah za Qur-aan tukufu; ni Mtume au nani?ur-aan kwenye msahafu au kusoma bila ya msahafu?

Jibu: Hatuna andiko kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) lenye kutolea dalili juu ya majina ya Suurah zote. Lakini hata hivyo kumethibiti baadhi ya Hadiyth Swahiyh kuzipa majina baadhi yake kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam); kama mfano wa al-Baqarah na al-´Imraan. Ama Suurah nyinginezo udhahiri ni kwamba zilipewa majina na Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum).

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (4/07)
  • Imechapishwa: 22/08/2020