Swali: Kuna Suufiyyah wanaowajuzishia watu kusujudu kwa asiyekuwa Allaah na wanatumia hoja kwa Malaika kumsujudia Aadam (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Vilevile wanasema kuwa wakimuona mtu anayesujudia kaburi hawamkufurishi mpaka kwanza wajue kilichomo ndani ya moyo wake. Ni vipi tutaraddi madai haya?
Jibu: Allaah (Jalla wa ´Alaa) aliwaamrisha Malaika wamsujudie Aadam Sujuud ya kuamkia na sio Sujuud ya ´ibaadah. Hii ni Sujuud ya kumkia na ikramu. Ndipo wakamsujudia kwa kutii maamrisho ya Allaah.
Allaah ametukataza kumsujudia asiyekuwa Yeye. Hivyo sisi hatumuasi Allaah na kumsujudia asiyekuwa Yeye na kuleta hoja ya kisa cha Malaika pamoja na Aadam. Jambo ni la Allaah na Allaah Yeye ndiye aliyewaamrisha Malaika ambapo Malaika wakawa wamemtii. Ama kuhusu sisi Allaah ametukataza kumsujudia asiyekuwa Yeye. Kwa hivyo hatumsujudii yeyote isipokuwa Allaah (Jalla wa ´Alaa).
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (20) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2130
- Imechapishwa: 09/07/2020
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)