Swali: Ni ipi hukumu ya muislamu wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah kumuoa mwanamke wa ki-Shiy´ah?

Jibu: Haifai kuoa kutoka katika Shiy´ah, kwa sababu miongoni mwao wapo wanaomwabudu ´Aliy, wanaomba msaada kwa watu wa familia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wanawashirikisha, wanawaomba badala ya Allaah. Hii ni shirki kubwa, khaswa Shiy´ah waliopo sasa ambao wengi wao duniani wanazidi kupindukia mipaka katika watu wa familia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Kwa hiyo kinachopaswa kwa Ahl-us-Sunnah ni kwamba asioe kutoka kwao isipokuwa ikiwa anajua kwamba yeye hayuko juu ya dini ya watu wake, kwamba ameingia katika Sunnah, amesimama imara juu ya Sunnah na ameacha yale waliyonayo watu wake ya kupindukia mipaka kwa watu wa familia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kwani wao hupindukia mipaka kwa watu wa familia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), wanamwomba ´Aliy badala ya Allaah, al-Husayn na Faatwimah na wanatafuta uokozi kwao, hata mwanamke wakati wa talaka husema ”Ee ´Aliy!”. Isipokuwa wale Allaah aliowataka, isipokuwa aliowaongoza miongoni mwao. Kwa hiyo inatakiwa kuhakikisha jambo hili. Tunamuomba Allaah atuongoze sisi na wao.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3391/حكم-زواج-السنة-من-الشيعة
  • Imechapishwa: 21/08/2026