Swali: Shangazi yangu mama wa mke wangu alimnyonyesha mtoto wa binti yake ambaye yuko na mume mwingine, lakini hajui idadi ya mara ngapi alinyonyesha. Mtoto huyu huingia kwa wasichana zangu na hawajisitiri mbele yake na anasema kuwa wao ni dada zake kwa kunyonya. Je, inathibiti hukumu ya kunyonya hali ya kuwa anayenyonyesha hajui idadi ya kunyonya? Hali ya kuwa mama wa mtoto anasema kwamba mama yake alimnyonyesha mtoto wake kwa muda wa siku tatu wakati wa ugonjwa wake. Je, yachukuliwe maneno ya mama wa mtoto au maneno ya anayenyonyesha?
Jibu: Lazima kwanza kuthibitisha kunyonya na iwe ni mara zisizopungua tano. Ikiwa anayenyonyesha ana shaka, basi maneno yake hayazingatiwi. Ikiwa ana shaka hajui ni tatu au mbili au nne au tano, basi maneno yake hayahesabiwi na wala kunyonya hakuthibiti kwa shaka. Ni lazima kama ilivyokuja katika Hadiyth ya ´Aaishah, lazima iwe ni mara tano zinazojulikana ndnai ya miaka miwili ya mwanzo. Hakuna kunyonya isipokuwa ndani ya miaka miwili. Kisha hayakubaliwi maneno yake wala ya mwingine isipokuwa ikiwa ni mwenye uadilifu, ikiwa mwanamke ni mwadilifu na anajulikana kwa uaminifu. Kwa msemo mwingine asiwe mwongo wala si muovu. Ama ikiwa ni mwongo au anajulikana kwa uovu, basi hayakubaliwi maneno yake. Ni mamoja iwe ni anayenyonyesha au asiye anayenyonyesha.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3383/شروط-ثبوت-الرضاعة
- Imechapishwa: 21/08/2026
Swali: Shangazi yangu mama wa mke wangu alimnyonyesha mtoto wa binti yake ambaye yuko na mume mwingine, lakini hajui idadi ya mara ngapi alinyonyesha. Mtoto huyu huingia kwa wasichana zangu na hawajisitiri mbele yake na anasema kuwa wao ni dada zake kwa kunyonya. Je, inathibiti hukumu ya kunyonya hali ya kuwa anayenyonyesha hajui idadi ya kunyonya? Hali ya kuwa mama wa mtoto anasema kwamba mama yake alimnyonyesha mtoto wake kwa muda wa siku tatu wakati wa ugonjwa wake. Je, yachukuliwe maneno ya mama wa mtoto au maneno ya anayenyonyesha?
Jibu: Lazima kwanza kuthibitisha kunyonya na iwe ni mara zisizopungua tano. Ikiwa anayenyonyesha ana shaka, basi maneno yake hayazingatiwi. Ikiwa ana shaka hajui ni tatu au mbili au nne au tano, basi maneno yake hayahesabiwi na wala kunyonya hakuthibiti kwa shaka. Ni lazima kama ilivyokuja katika Hadiyth ya ´Aaishah, lazima iwe ni mara tano zinazojulikana ndnai ya miaka miwili ya mwanzo. Hakuna kunyonya isipokuwa ndani ya miaka miwili. Kisha hayakubaliwi maneno yake wala ya mwingine isipokuwa ikiwa ni mwenye uadilifu, ikiwa mwanamke ni mwadilifu na anajulikana kwa uaminifu. Kwa msemo mwingine asiwe mwongo wala si muovu. Ama ikiwa ni mwongo au anajulikana kwa uovu, basi hayakubaliwi maneno yake. Ni mamoja iwe ni anayenyonyesha au asiye anayenyonyesha.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3383/شروط-ثبوت-الرضاعة
Imechapishwa: 21/08/2026
https://firqatunnajia.com/sharti-za-kuthibiti-unyonyeshaji/