Kutoa mimba ndani ya mwezi wa pili

Swali: Ni ipi hukumu ya kuavya mimba katika mwezi wa pili?

Jibu: Haifai kufanya hivyo isipokuwa kwa sababu inayokubalika katika Shari´ah.  Ama katika siku arobaini za kwanza wanazuoni wengi wanavumilia katika hilo ikiwa kuna maslahi, muda wa kuwa ndani ya arobaini za kwanza ni tone la maji. Ama ikiwa imeingia katika arobaini za pili, katika hatua ya damu iliyoganda na kipande cha nyama, basi lililo sahihi ni kwamba haijuzu isipokuwa kwa sababu ya Kishari´ah inayokhofiwa kutokana nayo juu ya mama.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3382/حكم-اسقاط-الحمل-في-الشهر-الثاني-فاكثر
  • Imechapishwa: 21/08/2026