Swali: Vipi kuhusu kuswali na viatu?
Jibu: Ni Sunnah, kujikurubisha na utiifu ikiwa viatu ni safi na salama. Lakini baada ya kuja mikeka hii ya kuswalia na watu wakaanza kuikanyaga na kuichafua, kwa sababu watu wengi hawajali viatu vyao wala hawavichunguzi, wavibebe na kuviweka sehemu maalum ili wasichafue mikeka ya watu. Kwa sababu watu wengi hawajali na hawachungi viatu wala hawana ufahamu katika jambo hili. Zama za mwanzo misikiti ilikuwa na kokoto na mchanga, na hilo halikuwa na madhara. Ni wajibu daima kwamba mtu asiingie msikitini isipokuwa kwa uangalifu na aangalie viatu vyake anapoingia msikitini ili visiwe na uchafu unaochafua msikiti, hata kama ni kokoto au machanga. Haifai kwake kuingia msikitini isipokuwa baada ya kuviangalia viatu na kuvigeuza ili aondoe uchafu uliopo, kisha akaswali navyo. Katika hali hiyo hakuna tatizo, kama Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alivyokuwa akiswali navyo. Lakini leo baada ya misikiti kutandikwa kwa mikeka ya thamani na kitu kidogo tu kinaweza kuiathiri, na huenda watu wakachukia kuswali juu yake na kuacha kuswali msikitini, basi inatakikana kwa muumini asiwaudhi watu. Bali awe msaada kwao katika kutekeleza swalah ya mkusanyiko na avihifadhi viatu vyake sehemu nyingine.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1009/مشروعية-الصلاة-بالنعال
- Imechapishwa: 08/01/2026
Swali: Vipi kuhusu kuswali na viatu?
Jibu: Ni Sunnah, kujikurubisha na utiifu ikiwa viatu ni safi na salama. Lakini baada ya kuja mikeka hii ya kuswalia na watu wakaanza kuikanyaga na kuichafua, kwa sababu watu wengi hawajali viatu vyao wala hawavichunguzi, wavibebe na kuviweka sehemu maalum ili wasichafue mikeka ya watu. Kwa sababu watu wengi hawajali na hawachungi viatu wala hawana ufahamu katika jambo hili. Zama za mwanzo misikiti ilikuwa na kokoto na mchanga, na hilo halikuwa na madhara. Ni wajibu daima kwamba mtu asiingie msikitini isipokuwa kwa uangalifu na aangalie viatu vyake anapoingia msikitini ili visiwe na uchafu unaochafua msikiti, hata kama ni kokoto au machanga. Haifai kwake kuingia msikitini isipokuwa baada ya kuviangalia viatu na kuvigeuza ili aondoe uchafu uliopo, kisha akaswali navyo. Katika hali hiyo hakuna tatizo, kama Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alivyokuwa akiswali navyo. Lakini leo baada ya misikiti kutandikwa kwa mikeka ya thamani na kitu kidogo tu kinaweza kuiathiri, na huenda watu wakachukia kuswali juu yake na kuacha kuswali msikitini, basi inatakikana kwa muumini asiwaudhi watu. Bali awe msaada kwao katika kutekeleza swalah ya mkusanyiko na avihifadhi viatu vyake sehemu nyingine.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1009/مشروعية-الصلاة-بالنعال
Imechapishwa: 08/01/2026
https://firqatunnajia.com/sunnah-ya-kuswali-na-viatu-hii-leo/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket