Swali: Je, kupiga chuku ni katika Sunnah?

Jibu: Ndio, akihitajia kufanya hivo. Imekuja katika Hadiyth:

“Hakika tiba bora mnazotumia ni kuumikwa na kuvuta dawa puani.”

Ameipokea Muslim.

Swali: Ni sehemu zipi ambazo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alifanyiwa chuku?

Jibu: Kilichojulikana ni kwamba alifanyiwa chuku kichwani mwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25359/هل-الحجامة-من-السنة
  • Imechapishwa: 07/03/2025