Kupokea malipo kwa kujitolea damu

Swali: Je, inafaa kumpa mtu malipo kwa kujitolea damu?

Jibu: Hapana, haifai. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kuuza damu na alikataza malipo ya damu. Kwa hivyo mtu hafai kuchukua chochote kama malipo yake.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25360/هل-تجوز-الاجرة-على-التبرع-بالدم
  • Imechapishwa: 07/03/2025